Tuesday, September 12, 2017

HABARI MBALIMBALI ZA MICHEZO NA BURUDANI


  • VYUO VIKUU EAC KUWA NA VIWANGO SAWA NA ADA⤦



  •  NYUMBANI KWA LISU MAPYA YAIBUKA!!!!!!!!!!!


  •  LOWASA ATUA KWA LISSU



⬅⬅⬅AGOMA KUPELEKA ORODHA YA WALIO HUKUMIWA



  • LWANDAMINA ATEMA CHECHE


BODI YA MIKOPO KUTANGAZA SIFA NA VIGEZO VITAKAVYOTUMIKA KUWAPANGIA WANAFUNZI MIKOPO 2017/2018


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema hivi karibuni itatangaza sifa na vigezo vitakavyotumika kuwapangia wanafunzi mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 unaotarajia kuanza miezi michache ijayo.


Ufafanuzi huo umetolewa jana (Ijumaa,
Julai 7, 2017) jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Dk Cosmas Mwaisobwa wakati akijibu maswali ya baadhi ya wateja waliotembelea Banda la HESLB katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere ambako HESLB inashiriki katika Maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara.

“Tunakamilisha mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka ujao wa masomo na tumepanga kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Julai tuwe tumeutangaza na tumefungua mtandao wetu ili waombaji wenye sifa waombe,” alisema Dk Mwaisobwa.

Dk Mwaisobwa amewataka waombaji wa mikopo watarajiwa wawe watulivu na kufuatilia kwa karibu vyombo vya habari na tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) ambayo huwa na kiunganishi (link) cha mfumo wa kuombea mkopo.

Awali, katika maonesho hayo, baadhi ya wananchi wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu wamepata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali yakiwemo tarehe ambayo Bodi itaanza kupokea maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Maswali mengine yaliyoulizwa ni kama utaratibu wa udahili kupitia vyuoni moja kwa moja utaathiri upatikanaji mikopo, wengine walitaka kupata elimu zaidi kuhusu taratibu za urejeshaji wa mikopo.

Akifafanua kuhusu maswali hayo, Dkt. Mwaisobwa alisema Sheria iliyoanzisha HESLB, pamoja na mambo mengine, inamtaka mnufaika kuanza kurejesha mkopo wake miezi 24 baada ya kuhitimu masomo.

Mkurugenzi huyo wa HESLB alisema kuwa sheria hiyo inamtaka mwajiri yeyote kuwasilisha kwa HESLB majina ya waajiriwa wake wote ambao ni wahitimu wa taasisi za elimu ya juu ndani ya siku 28 baada ya kuwaajiri na Bodi itamjulisha kama ni wanufaika au hapana pamoja na utaratibu na kiwango cha kumkata mnufaika.

Dk Mwaisobwa aliwataka wananchi kutembelea banda la HESLB kwa kuwa Bodi ya Mikopo itaendelea kuonyesha shughuli zake kwenye banda lake lililopo ndani, Banda la Benjamin Mkapa (Namba 19&20) hadi mwisho wa maonyesho hayo, tarehe 13 Julai, 2017.

TAMKO LA BARAZA LA HABARI,KUHUSU KUPIGWA RISASI MH.TUNDU LISSU




                        Siku tano zimepita tangu Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area D, Dodoma baada ya shughuli za Bunge September 7, 2017, Baraza la Habari Tanzania ‘MCT’ limesema limesikitishwa na jaribio hilo la mauaji.


  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kupitia kwa Katibu Mtendaji Kajubi Mkajanga leo September 12, 2017 Baraza hilo linaungana na wapenda amani na wadau wa habari na wa haki ya kujieleza na kutoa maoni kulaani kitendo hicho.


















                                                                                                                                                  



Monday, September 11, 2017

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI


Kuku wa kienyeji ni wazuri kwa ufugaji kwa sababu: Wanavumilia sana magonjwa, Ni rahisi kuwahudumia, Chakula chao ni cha bei ya chini, Wavumilivu wa hali tofauti za hewa, Hawahitaji uangalizi wa karibu, na soko lake ni kubwa sana na bei nzuri (Mayai trei moja SHs 10,000 mpaka 15,000, kuku wakubwa wanaanzia SHs 15,000 mpaka 30,000). Hii haimaanishi kwamba, uwaache kuku bila uangalizi, kwani nao hupata magonjwa kama wasipo patiwa chanjo sahihi, hupungua uzito na uzalishaji mayai hushuka kama wasipo patiwa chakula chenye virutubisho vyote. Hapa naelezea vitu muhimu katika hii formula ya ufugaji kuku wa kienyeji kwa mafanikio:

1. Aina ya kuku: Chagua aina ya kuku wenye uwezo wa kutaga mayai mengi na wakati huohuo, kuzalisha nyama nyingi. Hii itakupa faida kote, kwenye upande wa nyama na upande wa mayai. Kuku hawa wanajulikana kama Chotara, wanatabia sawa na kuku wa kienyeji wenye asili ya Tanzania wanaopatikana maeneo mengi nchini; kutokana na uvumilivu wao wa magonjwa na hali tofauti za mazingira. Pia wanauwezo wa kutaga mayai mengi (Wastani wa mayai matano kwa wiki) karibu sawa na kuku wa kizungu. Aina ya kuku hawa ni kama vile, Chotara wekundu (Rhode Island Red), Black Australorp (Weusi/Malawi), Barred Plymouth Rocks (Madoa), New Hamshire Red, Kuroila wanapatikana sana Uganda, na Kari kutoka Kenya. Hizi ni aina ya kuku zinazo patikana Tanzania.

2. Chanjo: Kama nilivyosema mwanzo, kuku wa kienyeji ni wavumilivu wa magonjwa lakini si kwamba hawayapati, kuna magonjwa ambayo ni hatari pia kwa kuku wa kienyeji. Chanjo ni muhimu kuwaepusha na hatari ya kuyapata magonjwa haya. Chanjo muhimu kwa kuku wa kienyeji ni; New Castle, Gumboro, Marek’s na Ndui ya kuku. Fuata utaratibu wa chanjo kutokana na ushauri wa daktari. Nitawaletea pia makala ya magonjwa na chanjo hivi karibuni.

3. Chakula: Kuku wa kienyeji pia wanahitaji mchanganyiko sahihi wa chakula, ili waweze kukupatia mazao mengi na bora, na kuwaepusha na magonjwa. Zipo fomula mbalimbali za chakula kutokana na umri wa kuku, na aina ya kuku. Kuku wote wanahitaji chakula chenye mchanganyiko sahihi wa Madini, Vitamini, Protini, Fats, Wanga, Vyakula vya kulinda mwili ili usipatwe na maradhi, na Maji safi. Muhimu kuwapatia kuku majani kama ziada ya chakula, hii hupunguza gharama za chakula na kuwafanya kuku waonekane wenye afya bora. Ni vizuri kuwapatia vifaranga chakula spesheli cha dukani kama huna ujuzi wa kutengeneza mwenyewe. Kwani vifaranga wengi hufa kutokana na kutokupata chakula chenye mchanganyiko sahihi kwao. Kuku wa mayai pia wanahitaji mchanganyiko sahihi ili waweze kutaga mayai kwa wingi.

4. Banda: Kuku wa kienyeji pia, wanahitaji banda au nyumba ya kuku imara ili kuweza kuwakinga na baridi kali, wanyama hatari, na wizi. Banda pia liwe na semu nzuri za kutagia na sehemu za kulala ziwe juu , kwani kuku hupendelea kulala juu. Ni muhimu banda liwe katika hali ya usafi muda wote. Kwa hivyo ni vizuri linyanyuliwe juu kidogo ili kuruhusu uchafu kuanguka chini na lijengwe ka kutumia mbao, mabanzi, milunda, nyavu, na mabati. Vifaranga wanahitaji kutenganishwa na kuku wakubwa. Banda si lazima liwe la gharama kubwa, kwani mafanikio ya ufugaji wa kuku ni vile unavyo waangalia na si banda. Mada inayohusu mabanda bora ya kuku itakuja hivi karibuni.

5. Majogoo kwa majike: Ili mayai mengi yaweze kutotolewa, ni vizuri jogoo mmoja aweze kuwahudumia majike wasio zidi 7. Kwani kuku wanaweza kutaga bila ya jogoo, lakini mayai hayatoweza kuleta kifaranga. Ili mayai yalete vifaranga ni lazima yawe yamerutubishwa (Fertilized eggs) na jogoo. Kwa hivyo ni vizuri kuweka Jogoo 1 kwa majike 7, hivyohivyo Jogoo 2 majike 14, Jogoo 3 majike 21, n.k. Pia hakikisha kuku wanao tumika kuendeleza kizazi ni wale wenye afya bora. 

6. Vyombo vya chakula:
 Hakikisha vyombo vya chakula ni visafi na vinawatosheleza kuku wote. Vyombo hivi ni vizuri vifanyiwe usafi wa mara kwa mara, ili kuwaepusha kuku na magonjwa. Maji machafu huwa ni chanzo kikuu cha magonjwa hasa ya kuhara. Hakikisha kuku wako wanabadilishiwa maji angalau mara mbili kwa siku.

KILIMO CHA NYANYA.





Nyanya ni zao la mboga linalolimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani. Kwa Tanzania, nyanya ni zao la kwanza katika mazao ya mboga linalolimwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha na mboga zingine. Nyanya hutumika karibu katika kila mlo. Kulingana na umuhimu wa zao hili kama chakula na pia kama zao linalomwingizia kipato mkulima, kuna haja ya kutoa mafunzo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wake.




Maeneo yanayolima nyanya
Inadhaniwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru au Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.



Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa ni kama; Malawi, Zambia na Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania.



Kwa upande wa Tanzania mikoa inayolima nyanya kwa wingi hasa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na biashara ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Iringa (Ilula), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida.
nyanya-zilizochumwa
Nyanya kwenye sahani

Mazingira yanayofaa kwa kilimo cha nyanya

Hali ya Hewa: Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa)



Udongo: Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 - 7.0.



Mwinuko: Nyanya hustawi vizuri kutoka sehemu za mwambao hadi kwenye mwinuko wa mita 400-1500 kutoka usawa wa bahari; yaani nyanda za chini kati hadi za juu kutoka usawa wa bahari. Nyanya zinazopandwa nyanda za juu sana hukumbwa na mvua za mara kwa mara ambazo huambatana na magonjwa ya jamii ya ukungu; kama Bakajani chelewa (Late Blight)

Aina za nyanya

Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawili:

  1. Aina ndefu (intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tengeru 97, Marglobe (M2009). Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Uvunaji wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji.
  2. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa)

Kulingana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawaili:


  1. OPV (Open Pollinated Variety) - Hizi ni aina za kawaida
  2. Hybrid - Chotara: Hizi ni nyanya zilizoboreshwa, aina hii zina mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.













HABARI MBALIMBALI ZA MICHEZO NA BURUDANI

VYUO VIKUU EAC KUWA NA VIWANGO SAWA NA ADA⤦   NYUMBANI KWA LISU MAPYA YAIBUKA!!!!!!!!!!!   LOWASA ATUA KWA LISSU ➨ ...